VVU na mtoto wako

HIV and your child [ Swahili ]

PDF download is not available for Arabic and Urdu languages at this time. Please use the browser print function instead

Jifunza jinsi watoto hupata VVU, jinsi inaathiri miili yao, na nini unahitaji kufanya kama mzazi kutunza afya ya mtoto wako kama iwezekanavyo.

Yamuhimu

  • Baadhi ya watoto hupata VVU kupitia mama zao wakati wa mimba, au wakati wa kunyonyesha mtoto, kupitia damu au bidhaa ambazo vina VVU, au VVU kupitia sindano au vifaa vya operacheni vilivyoambukizwa.
  • Mtoto akipata VVU, virusi vya VVU vinashinda na huharibu aina fulani za seli nyeupe za damu.
  • Nchini Kanada, watoto ambao wana VVU wanaweza kufurahia maisha ya kawaida na yenye afya wakienda kliniki, na kutumia madawa kama inapaswa.
  • Matatizo mengi yanaweza kuzuiwa na dawa kama VVU imetambuliwa mapema.

VVU in nini?

  • Kushambuliwa kwa seli na VVU
    VVU inaambatanisha na seli ya CD4, hupenyeza yaliyomo yake.

    VVU, maana yake ni ukosefu wa kinga mwilini ( Sema: IM-you-no-de-FISH-en-see) VVU hushambulia aina fulani za seli nyeupe za damu inayoitwa CD4 cell. Seli za CD4 hupigana na maambukizo. Seli za CD4 wakati mwingine zinaitwa T seli, seli msaidizi, au CD4 lymphocytes.

  • Seli za CD4 zilizoambukizwa, hutumiwa kutengeneza nakala zaidi ya VVU. Hii huharibu seli za CD4.

    VVU inapoingia katika seli za CD4, inatumia kiini kutengeneza nyingi zaidi kutoka yenyewe. Na katika utaratibu huu VVU huharibu seli ya CD4.

  • Bila matibabu, idadi ya seli za CD4 inapungua sana na mfumo wa kinga hudhoofisha.

    Wakati unapoendelea na virusi zaidi hufanywa, idadi ya chembechembe za CD4 inapunguka. Hii inasababisha mfumo wa kinga mwili kuwa dhaifu zaidi. Mfumo wa kinga dhaifu una uwezo wa chini kupambana na maambukizi mengine na aina fulani za kansa.

Tofauti kati ya VVU na UKIMWI

Maambukizo ya VVU maana yake ni kwamba virusi vya ukimwi vimo katika mwili wa mtu. Baadhi ya watu watabakia na afya nzuri na maambukizo yao kwa muda, maadam wengine wataugua mapema. Mara VVU hukiingia mwili wa mtoto wako, kamwe hutoka kamili. Watu wenye VVU katika damu yao wanaitwa kwamba wana VVU . [HIV positive]

Ukimwi maana yake ni Ukosefu wa Knga mwilini. Ukimwi ni hatua ya mwisho ya maambukizo a VVU, ambayo hufanyika wakati:

  • uwingi wa seli za CD4 umepunguka sana.
  • baadhi ya aina ya maambukizo makubwa ao kansa yanaongezeka .

Jinsi watoto wapata ukimwi

Watoto wanaweza kupata virusi kwa njia zifuatazo:

  • Watoto wengi wanapata VVU kutoka mama zao ambao wameambukizwa pia.. VVU vinapitishwa kwa mtoto wakati wa mimba wa mama yake, wakati wa kuzaliwa, au wakati wakumnyonyesha
  • Baadhi ya watoto hupata ukimwi kupitia damu au bidhaa ambazo vina VVU. Watoto wengine pia wanapata VVU kupitia sindano au vifaa vya operacheni vilivyoambukizwa. Hi, kwa kawaida, hutokea katika nchi ambapo usambazaji wa damu usiopimwa na vifaa na sindano havisafishwa vizuri na havikusukiwa katika maji ya moto mwingi.
  • Mawasiliano ya ngono yasiyo salama kwa vijana au watoto ambao wamedhulumiwa yanaweza kusababisha maambukizo ya VVU.
  • intravenous (IV ) matumizi yake yanaweza pia kusababisha maambukizo ya VVU wakati sindano imetumiwa na zaidi ya mtu moja. Dawa ya IV huingizwa ndani ya mwili kwa kutumia sindano.

Kuwa na mtoto ambaye ana VVU, inasema nini kwako na familia yako

Kama mtoto wako ana VVU, unapaswa kupimwa ili ujue kama una VVU au siyo. Kama wewe una VVU, watoto wengine wako na washirika wako wa ngono wanapaswa pia kupimwa. Pia unapaswa kutafuta huduma kwa ajili yako mwenyewe ili uweze kukaa mwenye afya ili umtunze mtoto wako na familia.

Mtoto wako na watu wa familia yako wote ambao wameambukizwa VVU wanapaswa kwenda mara kwa mara kwa mtaalamu katika kliniki ya kutibu ukimwi.

Matibabu kwa watoto wenye VVU

Matibabu mawili ya mhimu yanatolewa kwa watoto wenye VVU:

  • madawa ya kutibu ukimwi
  • madawa ya kuzuia maambukizo mengine

Dawa yanayotibu virusi vya ukimwi huzuia chembechembe za virusi kuongezeka mwilini. Madawa haya huitwa ARVs (anti-retrovirals); wakati yamechangwa, matibabu mara nyingi hujulikana kama madawa ya kurefusha maisha au tiba ambayo imechangwa, anti-retroviral aktiv tiba (HAART). Kufanya kazi vizuri, dawa hizo lazima zichukuliwe bila kuchelewa kunywa hata dozi moja.

Madawa mengine yanatumiwa ili yazuie maambukizo mengine.Hizi ni pamoja na madawa kama trimethoprim-sulfamethoxazole (Septra), yanayopewa kuzuia aina mbaya ya nimonia [pneumonia]. Siyo watoto wote wanahitaji madawa haya ya kuzuia maradhi. Yanapewa tu, wakati mfumo wa kinga wa mtoto ni dhaifu kutosha, haddi kuwezesha aina hizi za maambukizo .

Unatarajia nini wakati wa miadi ya watoto huko kliniki ya VVU

Watoto wote wanapaswa kutemebelea kliniki mara kwa mara kuangalia afya zao, kwa kawaida kila miezi 1-3. Mtoto atapimwa uzito na urefu wake kuona kama mtoto anakua vizuri. Mtoto wako anatachunguziwa na mwuguzi na daktari moja au zaidi kuangalia afya ya mtoto wako tangu ziara ya mwisho. Kiasi kidogo cha damu kitachukuliwa kuona hali ya mfumo wa kinga ya mtoto, uwingi wa virusi katika damu, na vipimo vingine yva afya kwa jumla.

Vipimo vya kufuatilia maambukizi ya VVU

Kila miezi 3-4, vipimo maalum vya damu vitafanyika ili kutahmini jinsi mtoto wako anakabiliana na maambukizi ya VVU. Vipimo mbili vitafanyika:

  • Viral load inahesabu idadi ya VVU katika damu
  • ‘CD4 cell count ‘ ni idadi ya chembechembe za seli za CD4. Inatujulisha mfumo wa kinga unaendeleaje. Idadi ya kawaida ya seli za CD4 kwa mtoto, hutegemea umri wa mtoto.

Watu wanaopatikana kuwaone wewe na mtoto wako huko kliniki

Pamoja na madaktari na wauguzi wa mtoto wako, hawa ni baadhi ya watu wengine unaweza kuzungumza nao huko kliniki:

  • Mfanyakazi wa kijamii anaweza kuzungumza nawe kuhusu mambo ya kihisia na ya familia na jinsi VVU huathiri familia yako. Mfanyakazi wa kijamii anaweza pia kuwasaidia na masuala kama vile matatizo ya pesa, gharama ya madawa, na masuala ya uhamiaji
  • Mtaalam wa lishe anaweza kujadili nawe kuhusu mahitaji ya lishe ya mtoto wako.
  • Mtaalam wa elimu anaweza kuzungumza na wewe kuhusu maendeleo ya mtoto wako na uwezo wake kujifunza shuleni.
  • Mtaalam wa mwili anaweza kutathmini maendeleo ya mtoto wako kutumia maungo yake, kama kutembea na kukimbia
  • Mtaalam wa kiakili atapatikana kutathmini heshima ya asili ya mtoto na kama yuko au siyo tayari kuambiwa kuhusu VVU.

Wataalamu wengine wengi wanapatikana katika hospitali, ikiwa wanahitajika. Zungumza na madaktari na wauguzi wa mtoto wako kuhusu wasiwasi zozote unazo kuhusu mtoto wako, kuona kwamba mtu yeyote wa watu hawa anaweza kukusaidia na utunzaji wa mtoto wako.

Utafanya nini kama mtoto wako ni mgonjwa kati miadi au una wasiwasi kuhusu madawa yake

Unapaswa kuwa na daktari wa familia au daktari wa watoto karibu kwako kwa huduma za afya za kawaida . Baadhi ya maswali yanaweza kujibiwa kwa kupigia simu kliniki ya mtoto wako au inaweza kujadiliwa wakati wa miadi ijayo. Matatizo mengine yakitokea maana yake ni lazima mtoto apate huduma za afya kwa haraka zaidi kwa Daktari, ama katika kliniki, ao daktari wa familia au kwa ofisi ya Daktari wa watoto, au hata katika idara ya dharura katika hospitali karibu na wewe.

VVU na afya ya mtoto wako

Nchini Kanada, watoto ambao wana VVU wanaweza kufurahia maisha ya kawaida na yenye afya wakienda kliniki, kwa kawaida, kwa huduma za afya na kutumia madawa kama inapaswa. Watoto wengi wanatambuliwa wakati hawana au wana dalili chache. Hii inaruhusu timu ya matibabu kuanza madawa, ikiwa inahitajika wakati huo, kuweka mtoto awe na afya nzuri.

Baadhi ya watoto hutambuliwa kuwa wana VVU nyuma sana, wakati tayari wanaumwa sana kwa sababu ya maambukizo. Baadhi ya watoto hawa hawana uwezo/ au wanaweza kufa. Hatujaona hii kutokea katika muda mrefu sana.

Aina ya matatizo yanayoonekana katika watoto ambao wana VVU

Kabla ya kutambuliwa na VVU, baadhi ya watoto huonekana wenye afya sana na hawana dalili yoyote ya kuambukizwa. Watoto wengine watapata matatizo madogo kama yafuatayo:

  • Kukua kwa shida au shida kupata uzito
  • Maambukizo ya ngozi, kifua, sikio, au tumbo (tumbo na matumbo)
  • Magonjwa ya kinywani
  • matezi ambayo yamevimba
  • kuharisha
  • homa
  • Kuchelewa kwa (kimwili, kihisia, na kiakili)

Watoto wengine watapata matatizo makubwa kama vile nimonia, uti wa mgongo, kifua kikuu, ubongo (ubongo uharibifu), au saratani. Dawa inaweza kuzuia mengi ya matatizo haya ikiwa maambukizo ya VVU yamepatikana mapema.

Rasilimali ya VVU

Kama una maswali au hoja yoyote, wasiliana na daktari wako au kliniki ya VVU. Kwa habari zaidi, tafadhali tazama yafuatayo:

Teresa Group

www.teresagroup.ca (Inapatikana kwa kiingereta tu)
416-596-7703

CATIE: Community AIDS Treatment Information Exchange

www.catie.ca (Inapatikana kwa kiingereta tu)


Last updated: December 17 2009