VVU na mimba

HIV and pregnancy [ Swahili ]

PDF download is not available for Arabic and Urdu languages at this time. Please use the browser print function instead

Kama wewe umeambukizwa VVU, jifunza jinsi baadhi ya madawa yanaweza kupunguza hatari ya kupitisha V VU kwa mtoto wako.

VVU in nini?

VVU, maana yak​e ni ukosefu wa kinga mwilini ( Sema: IM-you-no-de-FISH-en-see) VVU ni virusi vinayoambukia seli fulani za kinga za mwili wa binadamu. Inafanya kinga ya mwili wa mtu kuwa dhaifu baada ya muda. Hii inaweka mtu kwenye hatari ya maambukizo makubwa mengine.

Mke ambaye ameambukizwa na VVU, anaweza kuambukiza mtoto wake. VVU vinaweza kupitishwa kwa mtoto wakati wa mimba wa mama yake, wakati wa kuzaa, ao wakati wakumnyonyesha. Wanawake wengine hawajui kwamba wanavyo VVU, mpaka wapate mimba na wapimwe kwa VVU.

Kama umeambukizwa na VVU na una mimba, au unapanga kuwa na mtoto, ukurasa huu unaeleza njia ya kupunguza hatari ya mtoto kuambukizwa na VVU.

Mtoto wako ana uwezekano ndogo kuambukizwa VVU, ukipata huduma bora kabla ya, wakati wa, na baada ya kuzaa mtoto.

Kama una VVU, unapaswa kumwona mtaalamu wa VVU. Hii ni muhimu hasa kama wewe ni mjamzito, au unapanga kuwa na mtoto. Mtaalamu wako wa VVV atafanya yafuatayo:

  • Atakushauri juu ya mchanganyiko ya madawa salama na bora kabisa ya kutumia
  • kufuatilia kiasi cha virusi kwenye damu yako (viral load) wakati wa ujauzito kuhakikisha madawa yanafanya kazi.

Unapaswa pia kumwona Mtaalam wa mimba wakati wa mimba yako. Mtaalam wa mimba ni daktari wa kimatibabu ambaye amepata mafunzo maalum ya kuhudumia wanawake wakati wa ujauzito, uchungu na kujifungua, na w wiki chache za kwanza baada ya kuzaa.

Daktari wa familia yako au kliniki ambapo ulitambuliwa kuwa na VVU, wanaweza kukutumia kwenda kumwona mtaalamu wa VVU na Daktari wa wanawake wajawazito.

Dawa kwa VVU

Hakuna tiba ya VVU, lakini kuna madawa mengi ambayo yanaweza kukusaidia kuwa na afya nzuri. Dawa husaidia kudhibiti chembechembe za virusi kuenea mwilini na pia husaidia kulinda mtoto wako kuambukizwa na VVU.

Unaweza kufanya nini kama ulikuwa unachukua/ dawa ya VVU kabla ya kupata mimba

Wewe kuwa na afya nzuri ni muhimu sana kwa afya ya mtoto wako, lakini baadhi ya madawa siyo salama kwa ujauzito. Ikiwa tayari unachukua dawa ya VVU na unataka kupata mimba au kujua kama wewe ni mjamzito, basi, mjulisha mtaalamu wako wa VVU. Anaweza kusaidia kupendekeza madawa bora kwako.

Dawa hupunguza hatari kwa mtoto wako kuambukizwa na VVU

Kuchukua dawa ya VVU wakati wa ujauzito hupunguza hatari ya VVU kupitishwa kwa mtoto wako. Uchunguzi umeonyesha kwamba mwanamke akichukua madawa wakati yeye ni mjamzito na kiasi cha virusi mwilini ni ndogo wakati wa kujifungua, hatari ya kupitisha VVU kwa mtoto inakuwa ndogo sana. Mtaalamu wako wa VVU na Mtaalamu wako wa ujauzito wataendelea kupima kiasi cha chembe chembe za VVU yako wakati wa ujauzito. Hii itahakikisha kwamba madawa yako yanatumika vizuri na kwamba mtoto wako hataambukizwa.

VVU: Dawa na Kiasi cha chembe chembe za virusi mwilini

Vipimo kadhaa vya VVU katika damu bila dawa na kiini kimoja cha VVU katika damu na dawa
Kutumia dawa ya VVU husaidia kupunguza idadi ya virusi vya ukimwi katika damu. Kiasi cha virusi katika damu kinaitwa "viral load". Wakati ‘viral load’ ni ndogo, hatari ya kupitisha VVU kwa mtoto wako inapunguka sama

Lini na muda gani kuchukua dawa ya VVU hutegemea hali yako

Mtaalamu wako wa VVU hujadili na wewe majira ya dawa yako ya VVU

  • Kama unahitaji kuchukua dawa kwa afya yako mwenyewe, utaendelea kutumia dawa baada ya mtoto kuzaliwa
  • Baadhi ya wanawake hawahitaji dawa katika hatua yao ya maambukizi ya VVU. Kama huna haja yakutumia dawa ya VVU kwa afya yako mwenyewe, unapaswa kuanza kutumia dawa baada ya mwezi wa tatu wa ujauzito. Chukua tu mpaka mtoto kuzaliwa. Ongea na na Daktari wako wa VVU kuhusu lini kuacha kutumia dawa.

Kadhaa ya madawa ya VVU ni salama kwa ujauzito

Baadhi ya madawa ya VVU ni salama kabisa katika ujauzito. Hayo ni pamoja na madawa kama zidovudine (AZT), Lamivudine (3TC), na lovinapir / ritonavir (Kaletra). Madawa mengine yametumika katika kipindi na madawa ya karibu zaidi yanatumika mara nyingi zaidi. Baadhi ya madawa ni dhahiri si salama kwa ujauzito. Mtaalamu wako wa VVU anaweza kusaidia kupendekeza dawa salama na bora kabisa kwa ajili yako.

Kuzaa kwa njia ya kawaida dhidi ya caesarean section (C-section) Kuzaa kwa njia ya kupasuliwa

Kama kiasi cha virusi wako ni kubwa kuliko 1000 wakati wa kujifungua, upasuaji wa C-Section itapunguza hatari ya kupitisha VVU kwa mtoto wako. Idadi kubwa ya virusi inaweza kutokea kwa sababu hizi zifuatazo:

  • kama madawa hayakandamize virusi kabisa
  • kama wewe ulichelewa kuchukua dawa katika ujauzito
  • kama wewe huchukuwe dawa mara kwa mara

Kama idadi/kiasi cha virusi wako ni chini ya 1000, C-section haifanyi mtoto wako kuwa na salama hata kidogo. C-section si salama pia kwa wewe kuliko kujifungua kwa kawaida (kwa njia ya uke). Kwa sababu hii, ikiwa idadi ya virusi wako ni mdogo wakati wa uchungu, unapaswa kuwa na uwezo wa kujifungua kwa kawaida.

Jadiliana na mtaalamu wako wa VVU na mtaalam wako wa ujauzito kuhusu aina gani ya kujifungua ni bora kwako.

Utafanya nini ukianza na uchungu

Endelea kuchukua madawa yako, hata wewe uko katika uchungu. Nenda hospitali baada unashuku wewe ni katika ajira. Utapaswa kupewa moja ya madawa unatumia (AZT) kwa kupitia veni (IV) [mshipa wa damu], wewe. IV maana yake ni dawa linaloingiziwa ndani ya veni. Ni bora kulipokea angalau masaa 2-4 kabla ya mtoto aje.

kutoa dawa kwa kupitia kinywa

Utambulisho wa mitochondria katika seli

Utatarajia nini wakati mtoto wako amezaliwa

Mtoto akizaliwa, mtoto ataanza kutumia AZT ndani ya masaa 24 ya kwanza ya maisha. Utahitaji kumpatia mtoto wako dawa hii mara nne kwa siku, kwa wiki sita za kwanza za maisha yake. Hii inaweza kupunguza zaidi hatari ya maambukizo ya VVU kwa mtoto wako.

Mtoto wako pia atahitaji kupimwa damu kwa VVU

Usimyonyesha mtoto wako. Kunyonyesha ni njia moja ya kupitisha VVU kutoka kwa mama hadi mtoto. Uji wa watoto ni chakula salama kwa mtoto wako.

Kwa habari zaidi, tafadhali soma "VVU na mtoto mchanga wako."

Kwa habari zaidi

Kama una maswali au hoja yoyote, wasiliana na daktari wako au kliniki ya VVU. Kwa habari zaidi, tafadhali tazama yafuatayo:

Motherisk

www.motherisk.org (Inapatikana kwa kiingereta tu)

CATIE: Community AIDS Treatment Information Exchange

www.catie.ca (Inapatikana kwa kiingereta tu)

Yamuhimu

  • Wanawake wajawazito ambao wameambukizwa virusi vya VVU inapaswa kuchukua madawa ya kupunguza hatari ya kupitisha VVU mtoto wao.
  • Kama unatumia madawa na chembe chembe za virusi wako ni mdogo wakati wa kujifungua, hatari ya kupitisha VVU kwa mtoto wako inakuwa ndogo sana.
  • Kama chembe chembe za virusi wako ni mkubwa kuliko 1000 wakati wa kujifungua, C-section hupunguza hatari ya kupitisha HIV kwa mtoto wako.
  • Kama chembe chembe za virusi wako ni chini ya 1000, C-section haitoi faida yoyote kwa mtoto wako. Unapaswa kuwa na uwezo wa kujifungua kwa njia ya kawaida (uke).
Last updated: Desemba 17 2009