VVU na mtoto mchanga wako

HIV and your baby [ Swahili ]

PDF download is not available for Arabic and Urdu languages at this time. Please use the browser print function instead

Kujifunza jinsi ya kupunguza hatari ya kupitisha HIV mtoto wako na jinsi daktari anaweza kujua kama mtoto wako ana VVU mara moja yeye kuzaliwa.

VVU in nini?

VVU, maana yake ni ukosefu wa kinga mwilini ( Sema: IM-you-no-de-FISH-en-see) VVU ni virusi vinayoambukia seli fulani za kinga za mwili wa binadamu. Inafanya kinga ya mwili wa mtu kuwa dhaifu baada ya muda. Hii inaweka mtu kwenye hatari ya maambukizo makubwa mengine

Watu ambao wameambukizwa na VVU huitwa HIV-positive. Watu ambao hawakuambukizwa na VVU huitwa HIV-negative.

Watoto wengi wanao VVU huipata kutoka kwa mama zao ambao wamebukizwa pia. VVU hupitishwa kwa mtoto wakati wa ujauzito, wakati wa kuzaliwa, au kwa njia ya kunyonyesha. Kama wewe una VVU na unatarajiya kuwa na mtoto,ukurasa huu unaeleza jinsi ya kupunguza uwezekano kwa mtoto wako kupata VVU na jinsi ya kung’amua kama mtoto wako amembukizwa.

Mtoto wako ana uwezekano ndogo kuambukizwa VVU, ukipata huduma bora kabla ya, wakati wa, na baada ya kuzaa mtoto.

Wanawake wajawazito wote au wanawake ambao wanafikiria kupata mimba, wanapaswa kupimwa VVU.

Kama mwamke mjamzito ana VVU na hapati dawa wakati wa ujauzito au kujifungua, hatari ya kuambukizwa kwa mtoto ni karibu 25%. Hii ina maana 1 wa watoto 4 ataambukizwa.

Hatari kwamba mtoto wako ataambukizwa na VVU itakuwa ndogo sana ikiwa kama hivi vyote vifuatavyo vimefanyikiwa:

  • Unachukua dawa baada ya miezi 3 ya kwanza ya ujauzito wako na/kiasi cha virusi hakionekani, maana yake kuna virusi vyaVVU vichache tu katika damu yako hawawezi kupatikana katika vipimo.
  • Wakati wa uchungu, unaweza kupata dawa liitwayo zidovudine (AZT) kupitia intravenous (IV) line, njia ya mshipa). Hii ina maana dawa huingia moja kwa moja kwenye damu yako kupitia veni.
  • Baada ya kuzaliwa, mtoto wako anachukua AZT kwa wiki 6.

Kama mambo haya yote hufanyika, basi hatari ya kuambukizwa mtoto wako ni chini ya 1%. Hii ina maana kuwa wachache kuliko 1 kwa watoto 100 wataambukizwa.

Kwa habari zaidi, tafadhali soma "VVU na mimba."

Mtoto atahitaji kupimwa kwa VVU

Daktari hawezi kujua kama mtoto wako ana VVU kwa kumuangalia tu. Mara nyingi watoto wanao VVU, hufanana na watoto ambao hawana VVU. Kama mtoto anaumwa ma maambukizo mengine, hii inaweza kuhusiana na VVU. Inaweza pia kuwa maambukizo ambayo yangeweza kutokea kwa mtoto kwa njia nyingine.

Vipimo vya VVU

Daktari wa mtoto wako anahitaji kupima damu ya mtoto wako baada ya kuzaliwa na mara 2 zaidi, kwa kawaida wakati mtoto wako ana umri wa mwezi 1 na umri wa miezi 2. Kipimo hiki kinaitwa PCR, ambayo inafanywa kwa Polymerase Chain Reaction, Inatafuta VVU katika damu ya mtoto wako. Inachukua muda wa mwezi 1 ili kupata matokeoya kipimo. Ikiwa vipimo vya PCR havipati virusi vyovyote, mtoto wako hakuambukizwa na VVU.

Kwa watu wazima na watoto wakubwa, kipimo cha kawaida cha VVU ni kipimo cha chembe chembe za kinga [antibodies]. Kinga ya mwili ya binadamu hufanya Chembe chembe za kinga kusaidia kupigana na maambukizo. Wakati mtoto ana uambukizo au anapata chanjo, mwili wake hufanya antibodies dhidi ya maambukizo hayo. Kama mtu ana antibodies vya VVU katika damu yake, maana yake kwa kawaida ni ana VVU. Hivyo, kipimo cha antibody kinatafuta antibodies za VVU katika damu. Mjuwe ya kwamba antibodies za VVU hazilinde kamwe dhidhi ya VVU.

Kipimo cha antibody hakitumike kwa wachanga. Wakati mwanamke ni mjamzito, yeye anapitisha mwenyewe baadhi ya antibodies zake kwa mtoto wake. Hii ina maana kwamba kama mwanamke ana VVU, kipimo cha antibody daima kitaona VVU antibodies katika damu ya mtoto wake, hata kama mtoto hana VVU. Kwa sababu hii, mtoto wako atahitaji badala kipimo cha PCR kuona kama ana virusi vya ukimwi katika damu yake.

Antibodies za VVU zinavuka Placenta

Mtoto anapokea dawa kwa mdomo kupitia sirinji
Damu ya mama haichanganye na ya mtoto katika placenta. Antibodies za mama zinazopambana dhidhi ya VVU zinaweza kuvuka placenta, lakini kwa kawaida virusi ya VVI haviwezi. Kwa hiyo, kipimo cha antibody kwa watoto wachanga hakiwezi kupima kwa usahihi ukuwepo wa VVU kwa watoto.

Mtoto wako atahitaji kutumia dawa ya AZT

Mtoto akizaliwa, mtoto ataanza kutumia AZT ndani ya masaa 24 ya kwanza ya maisha. Utahitaji kumpatia mtoto wako dawa hii mara nne kwa siku, kwa wiki sita za kwanza za maisha yake. Hii inaweza kupunguza zaidi hatari ya maambukizo ya VVU kwa mtoto wako.

kutoa dawa kwa kupitia kinywa

Utambulisho wa mitochondria katika seli

Usimnyonyesha mtoto wako

Kama una VVU, usimnyonyeshe mtoto wako. Kunyonyesha ni njia moja ya kupitisha VVU kutoka kwa mama hadi mtoto. Nchini Kanada na zingine zilizoendelea, formula ni aina ya lishe salama kwa mtoto wako. Kuna mradi katika Ontario unaotoa bure formula kwa mwaka wa kwanza wa maisha ya watoto ambao wamezaliwa na mama wanao VVU. Wasiliana mradi kwa kupigia simu Teresa Group. Kama uko nje ya Ontario, muulize mtoa huduma ya afya wako kuhusu miradi ya kutoa bure formula

Mtoto wako anaweza kuwa na madhara kutoka madawa

Hata kama mtoto hana virusi vya ukimwi, daktari atafuata mtoto wako ili kuona kama dawa yanasababisha matatizo yoyote ya muda mfupi au mrefu. Dawa yaliyopewa mama wajawazito ni salama sana. Matatizo chache ya dawa huonekana kwa muda mfupi.

  • AZT inaweza kusababisha anemia katika mtoto wako baada ya kuzaliwa. Anemia maana mtoto wako hana chembechembe nyekundu za damu za kutosha, seli zinazo beba oksijeni kwa mapumziko ya mwili.
  • AZT inaweza pia kuharibu mitochondria na kusababisha mtoto kuwa na matatizo ya damu au ini. Mitochondria zinapatikana katika mwili wako wote(say: my-toe-KON-dree-uh) . Zinatowa msaada wakufanya nishati katika mwili.

Anemia yoyote au uharibifu kutoka mitochondrial kawaida unakwenda mara tu kusimamishwa.

Mitochondria

Seli zina unity ndogo ambazo zinaitwa maalum organelles ambazo zina utendaji maarufu. Mitochondria ni Organelles zinazo amua kama nishati ya viwanda

Hadi sasa, tafiti zinaonyesha kuwa kutumia dawa hizi haina madhara ya muda mrefu. Pia tafiti zinaonyesha kwamba watoto wakipata madawa haya ni kawaida.

Tutathmini maendeleo ya mtoto wako kwa kiwango kawaida. Kama inasababisha wasiwasi wowote,tutakuomba kufwata mipango mingine ya huduma

Kama mtoto wako ana virusi vya ukimwi

Nhini Kanada, watoto ambao wana VVU wanaweza kuwa na afya, maisha ya kawaida kama wanakwenda kliniki mara kwa mara kwa ajili ya huduma ya afya na kuchukua madawa kama eda. Kama mtoto wako amekutwa mapema, daktari anaweza kuanza kumpa madawa hapo hapo, kama inahitajika, ili kutunza afya yake.

Kwa habari zaidi, tafadhali soma "VVU na mtoto wako."

VVU na rasilimali ya mamba

Ikiwa una maswali yoyote au wasiwasi, wasiliana na daktari wa mtoto wako au kliniki ya VVU.

Kwa habari zaidi, tafadhali tazama yafuatayo:

Motherisk

www.motherisk.org (Inapatikana kwa kiingereta tu)

Teresa Group

www.teresagroup.ca (Inapatikana kwa kiingereta tu)

416-596-7703

Yamuhimu

  • Mmoja katika watoto wa 4 ambao wa mama wao wana VVU ameambukizwa VVU kama mama hakupata dawa wakati wa ujauzito au kujifungua.
  • Madawa kwa wote mama na mtoto huweza kupunguza hatari ya mtoto pia kupata VVU.
  • Mtoto wako atahitaji huduma ya kufuatilia ili kuona kama madawa hayatasababisha madhara yoyote.
Last updated: 十二月 17 2009